Monday, February 8, 2010

Madhumuni Ya Blog Ya Mafanikio Na Utajiri


Utangulizi: Mafanikio Na Utajiri

Umezaliwa ili Ufanikiwe! Kila anayetaka anaweza kufanikiwa. Yeyote atakayekwambia tofauti na hili atakuwa hana ufahamu juu ya kanuni za mafanikio.


Blog hii ni ya kuelimishana na kubadilishana mawazo juu ya nini kifanyike katika maisha ili mafanikio yapatikane, na pia ni kwa namna gani mtu yeyote anaweza kuwa tajiri kwa kufuata utaratibu au sheria za kisayansi ambazo zimekwisha thibitishwa.



Kabla ya kuendelea inatupasa tujiulize kwa uhakika kuwa mafanikio ambayo utajiri ni moja ya sehemu mojawapo ni nini hasa? Ieleweke kuwa tunapoongelea mafanikio, tunaangalia maisha yetu kwa ujumla, tunakotoka, tulipo na tunakoelekea.



Unaweza kufanikiwa katika maisha kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

  • Kufanya jambo jema ambalo hakuna mwingine aliyelifanya
  • Kutoa zaidi kwa wenye shida na wahitaji kuliko kupokea
  • Kama wewe ni bingwa au mshindi wa jambo fulani
  • Kama unayo furaha ya kweli na amani kuliko huzuni


  • Kama unatumia muda mchache kufikiria juu ya watu wengine kuliko wao wanavyokufikiria wewe
  • Kama wewe unatenda mema na muda wako wa kufa ukifika huogopi
  • Kama utakumbukwa hata miaka 100 baada ya wewe kutoweka


  • Kama utaleta tofauti ya mtu yeyote katika kuboresha maisha yake
  • Kama utapata mtu au mwenzi ambaye atakupenda kweli na kwa dhati
  • Kama ukifanya kila likupasalo kutenda na hata zaidi
  • Kama hukumuumiza yeyote kwa makusudi
  • . . . . .
Ukweli ni kuwa hakuna orodha kamili au hata alama zitakazokuonyesha kuwa wewe umefanikiwa au la. Hata hivyo, ziko njia fulani na dondoo ambazo zinaweza kukusaidia uweze kufikia katika ngazi fulani ya maisha yako.



Blogu hii ya Mafanikio ingependa kuyaleta mambo mbalimbali ambayo kama tutayazingatia yanaweza kusaidia kuweka msingi katika mafanikio ya maisha yetu au yale tuliyokusudia kuyafanya.

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe
Continue Reading...

Followers

News And Updates

Sign up to receive news as well as receive other blog updates!

Enter your email address:

Follow The Author